Michezo

Gabon yatia fora ufunguzi wa Afcon U-17

Mwenyeji wa mashindano ya  Fainali za vijana wa umri chini ya miaka 17 Afcon, timu ya taifa ya Gabon wameyaanza mashindano vibaya hapo jana,  baada ya kukubali kipigo cha Magoli 5 kwa 1 kutoka kwa timu ya taifa ya Guinean mchezo ambao ulikuwa wa ufunguzi .

Katika mchezo huo wa kundi “A” ,ufunguzi wa Fainali za vijana Afrika timu ya Guinea iliifunga rumbesa hilo la magoli Gabon katika uwanja wa Uwanja wa Port Gentil . Wachezaji walioing’arisha timu ya Vijana wa Guinea katika mchezo huo ni Djibril Toure alifunga dakika ya sita na 70, Nahodha Sekou Camara alie ipatia timu yake goli dakika ya 30, Elhadji Bah dakika ya 36 na Aguibou Camara dakika ya 45, huku goli pekee la kufutia machozi la Gabon  lilifungwa na mchezaji alietokea benchi ,Fahd Moubeti .

Katika michezo hiyo ya Kundi  “A” ,Mabingwa wa kihistoria timu ya taifa ya Ghana  walichanga vyema karata zao na kuchomozana ushindi wa magoli 4 kwa 0  dhidi ya Cameroon  mchezo ulipigwa katika Uwanja wa Port Gentil, mabao ya Nahodha Eric Ayiah na kiungo Ibrahima Sulley kila mmoja mawili.

Hii leo kutakuwa na michezo miwili ya kundi B, Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inaingia uwanjani  katika mchezo wake wa kwanza wa michuano hiyo.
Tanzania watapimana ubavu na mabingwa watetezi timu ya Taifa ya Mali huku Timu ya taifa ya Angola nao wakitupa karata yao kuwa vaa Niger michezo itakayo pigwa  katika Uwanja wa l’Amitie Sino mjini Libreville nchini Gabon.

BY HAMZA FUMO

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents