Burudani

Galatone kuwasha moto Dedee Fashion Morogoro

Msanii wa muziki Galatone atakuwa mmoja kati ya wasanii ambao watapamba onyesho la mitindo, Dedes Fashion linalotarajiwa kufanyika weekend hii (Julai 30) katika ukumbi wa Mambo Club, Morogoro ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mrogoro.

Akiongea na waandishi wa habari Jumatatu hii Mkurugenzi wa Dedee Fashion, Abdalah Ng’itu alisema mpaka sasa maandalizi ya onyesho hilo yanaenda vizuri huku akiwataka wakazi wa Morogoro kuhudhuria onyesho hilo lenye burudani za kila aina.

“Tunamshukuru Mungu maandalizi yanaendelea vizuri, kila kitu kinaenda sawa. Kikubwa tunaomba watu wajitokeza kwa wingi kwa sababu hili ni onyesho la vijana ambalo linaenda kuonyesha jinsi vijana wanavyoweza kutumia sanaa zao kama ajira. Rais Magufuli anawataka watanzania wafanye kazi, sisi tumeona tusisubiri tuajiriwe na mtu fulani, tumeona kama vijana kwa pamoja tujikusanye na kuonyesha vipaji vya sanaa tulivyonavyo,” alisema Ng’itu.

Aliongeza,”Kwahiyo hili tulio litakuwa na burudani mbalimbali kama mnavyosikia matangazo, Dedee Fashion itaonyesha mavazi yake, kutakuwa na red carpet, yaani ni show ambayo inakuwa na mambo mengi mazuri na yakuvutia. Kwahiyo tunaomba vijana wajitokeze kwa wingi ili tuunge mkono vya nyumbani,”

Pia katika onyesho hilo wabunifu mbalimbali wa Morogoro watapata fursa ya kuonyesha mavazi yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents