Burudani

Galaxy adai jina lake lilimgombanisha na familia yake

Kila msanii anaweza akawa na stori kubwa kupitia jina lake analolitumia kwenye sanaa – Lakini kwa Galaxy jina hilo huwa linamtoa machozi kwa kukumbuka jinsi ilivyosambaratisha.

Muimbaji huyo wa Top In My Heart, ameiambia Bongo5 kuwa alipewa jina hilo na baba yake mzazi, ambaye alitengana na mama yake baada ya na baadaye alilazimishwa kubadili jina hilo.

“Jina la Galaxy nilipewa na baba yangu mzazi ambaye alilipenda jina hilo kutokana na rafiki yake aliyeishi Uingereza kutumia jina hilo. Baada Ya wazazi wangu kutengana na mimi nilichukuliwa na mama, babu yangu mzaa mama hakulipenda hili jina na akalibadilisha na kuniita Rashid,” amesema.

“Baada ya baba yangu kufariki nikaamua kumuenzi mzazi wangu huyo kwa kulitumia jina lile la zamani. Ilileta ugomvi kwenye familia lakini hatimaye waliweza kunielewa,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents