Game gumu, wakongwe wajipange

Game gumu, wakongwe wajipange
Msanii
Jafari Ally Mshamu a.k.a Jaffarai ambaye bado anang’aa na ngoma yake
‘Napenda nini’ juzi alitamka kwamba wasanii wengi wa Bongo Flava
waliowahi kukimbiza siku za nyuma wanashindwa kurudi kwenye game
kwakuwa hawajipangi.

Msanii huyo alisema kwamba, ili msanii
uweze kurudi vizuri kwenye game baada ya kukaa kimya muda mrefu inabidi
ujipange kwa kufanya kazi bora vinginevyo kila ukitaka kutoka unapotea
tena kwakuwa game la muziki hivi sasa imekuwa na changamoto kubwa hasa
kutoka kwa chipukizi wengi wanaoibuka kunako tasnia hiyo.“Si unaona
mimi ninavyofanya kazi zangu, huwa nakaa muda mrefu bila kusikika,
lakini ninaporudi nakuwa kivingine zaidi kitu ambacho kinaendelea
kuniweka juu. Wasanii wenzangu wa kitambo ambao wapo kimya kwa muda
mrefu na wanaotamani kurudi kwenye game letu wajaribu kufanya kazi
zenye ubora ambazo zitawafanya waonekane wapya,” alisema Jaffarai.

Kuhusu
game lake la muziki, Jaffarai alisema kwamba, kinachofuata baada ya
kutoka na ngoma yake, ‘Napenda nini’ aliyomshirikisha Fatma ni ngoma
yenye jina la ‘Saa Nyingine’ ambayo pia imefanyika kupitia studio za
Fish Crab chini ya ‘prodyuza’ Lamar. “Ndani ya ngoma hiyo
nimemshirikisha Naaziz kutoka Kenya, huo utakuwa ni utambulisho wa
albamu yangu mpya yenye jina la ‘Wali Nazi’ itakayokuwa na jumla ya
kazi kumi zikiwemo Msijisahau, Jaffaryhmes, Saa Nyingine, Napenda Nini
na nyingine kibao”.

Pia mchizi alisema kwamba, akiwa ni mmoja
kati ya wakali wa muziki huo wanaounda kundi la ‘Wateule’, siku chache
zilizopita wameachia wimbo mpya wa kundi ambao unakwenda kwa jina la
‘Msela’ ukiwa pia ni utambulisho wa albamu yao ambayo pia imekamilika.
“Kazi tumefanya mimi, Mchizi Mox, Jay Moe na Solo Thang ambaye bado
yuko Uingereza,” alisema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents