Burudani

Game imegharimu shilingi ngapi? Navy Kenzo wajibu (Video)

Wakati naongea na Navy Kenzo niliwatania kuwa mtu akiona video ya wimbo wao ‘Game’ waliomshirikisha Vanessa Mdee, lazima atagundua kuwa akaunti zao za benki zitakuwa zimeyumba kwa kiasi kikubwa kutokana na bajeti ya video hiyo iliyoongozwa na Justin Campos wa kampuni ya Gorilla Films ya Afrika Kusini.

“Kila kitu pale kinalipiwa,” alisema Aika, mmoja wa member wa kundi hilo linaloundwa na yeye pamoja na mchumba wake, Nahreel.

“Kuanzia location, character hamna mtu pale hajalipwa, hamna gari ambalo halijalipiwa, kila kitu kinaenda kwa bajeti. Hatutaja bajeti ni shilingi ngapi lakini tunaelewa kabisa mtu akiona ataona video imegharamikiwa,” aliongeza.

Nahreel anasema kufanya kazi na muongozaji wa video hiyo, Justin Campos na mke wake Candice Campos kumewaweka karibu zaidi na ni watu wazuri kufanya nao kazi.

“Sasa wale ni zaidi ya marafiki, tumeshakuwa kama familia, tunazungumza nao vizuri na wako very organised. Hawataki mtu uwe disappointed. Kwahiyo muda wote wanaanda vitu kama presentation fulani kwenye paper ambayo inakuelezea kila kitu. Kwahiyo unajisikia upo in a very friendly environment,” anasema Nahreel.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents