Michezo

‘Game’ ya Yanga na Simba wachezaji kutopeana mikono, marufuku hiyo kuanza leo mechi za Ligi Kuu

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limetangaza utaratibu wa wachezaji kutopeana mikono kabla ya kuanza kwa mechi na badala yake kutakiwa kusasilimiana kwa ishara pekee.

Kauli hii ya TFF inakuja baada ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu kutosalimiana kwa kupeana mikono ikiwa ni kama sehemu ya kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

”Utaratibu wa wachezaji kupeana mikono kabla ya kuanza mechi hautatumika kwa sasa, na badala yake watasalimiana kwa ishara tu.” Taarifa iliyoandikwa na TFF

Shirikisho hilo lenye dhamana ya kusimamia mchezo wa soka nchini limeongeza kuwa ”Utekelezaji huo unaanza leo katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zitakazochezwa kwenye viwanja mbalimbali.”

”Maelekezo hayo yanahusu pia mechi zinazoendeshwa na wanachama wa TFF pamoja na wanachama wao. Hatua hiyo ni utekelezaji wa ushauri uliyotolewa na Wizara ya Afya ikiwa ni tahadhari ya kujilinda na dhidi ya virusi hatari vya corona vinavyoendelea kusababisha taharuki kote duniani,” Mwisho wa maelezo ya TFF.

Kwa kuwa utaratibu huo utaanza leo kwenye mechi za Ligi Kuu basi itakuwa hivyo mpaka kwa michezo ijayo ukijumuisha ule wa Watani wa Jadi wa Yangasc na Simbasc unaotarajiwa kupigwa tarehe 8/ 03/ 2020 siku ya Jumapili .

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents