Habari

Gangnam Style ya PSY yafikisha views milioni 270+ kwenye YouTube ndani ya miezi miwili

Ni rahisi sana kuwa maarufu Marekani kama tu ukiwa na kitu tofauti cha kufurahisha. Mkorea Kusini PSY amejikuta nyota duniani kote kwa video ya wimbo wake ‘Gangnam Style.

Hata hivyo PSY anayaona mafanikio yake kama ndoto na anaogopa kuiamini kama Jim Carrey kwenye “The Truman Show.”

PSY akiwafundisha Britney Spears na Ellen kucheza Gangnam styke

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Seoul alisema alitokwa na machozi kwa kutoamini baada ya wimbo wake kuingia kwenye chart za Billboard 100 mapema mwezi huu.

Jamaa huyo mwenye miaka 34 sasa amesema atavua nguo zote kama “Gangnam Style” ikishika nafasi ya kwanza kwenye chart hizo. Wimbo huo kwa sasa umekamata nafasi ya 11.

Kevin Hart na Psy wakicheza kwenye MTV VMAs 2012

Uchezaji kwenye video hiyo tayari umeshaigizwa na watu kibao duniani na kuendelea kumpanisha chart msanii huyo.

Hadi leo “Gangnam Style”imeshaangalia zaidi ya mara milioni 270 kwenye YouTube ndani ya miezi miwili na bado namba inapanda.

Kwenye filamu ya mwaka 1998 ya “The Truman Show,” Carrey anaigiza kama mtu asiyejua kuwa anaishi kwenye reality television show.

Kama bado hujaiangalia video hiyo icheck hapa:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents