Burudani

Gangnam Style yamaliza utemi wa Justin Bieber kwenye YouTube

Justin Bieber amekuwa akiitawala YouTube kwa muda mrefu tangu aanze kwa kuupload video zake mwenyewe kipindi hajawa maarufu mpaka siku chache zilizopita ambapo amepatikana mbabe mwingine.

Na sasa The Biebz wamepoteza taji lao la “King Of Youtube” kwa muimbaji wa kikorea kusini Psy, ambaye ameivunja rekodi ya Justin kwenye mtandao wa Youtube!

Mfalme huyo mpya wa Youtube ameipiku video ya Justin ya wimbo wake “Baby” kwa video ya wimbo wake uliojipatia umaarufu mkubwa duniani “Gangnam Style” kwa kuwa video iliyoangaliwa zaidi kwenye mtandao huo tangu uanzishwe.

Wakati Justin akiwa na views milioni 803 na kitu, Gangnam Style imefikisha views milioni 805 na zaidi.

Cha kushangaza zaidi ni kuwa Psy ameifikia rekodi hiyo miezi minne tu tangu iingie kwenye internet.

Kwa mafanikio hayo, msanii huyo aliamua kujipongeza kupitia Twitter kwa kuandika:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents