Michezo

Gareth Bale aifungia Wales goli muhimu katika michuano ya Ulaya

Timu ya taifa ya Wales huenda ikawa imechungulia kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Ulaya baada ya kushindwa kufuzu kwa takribani miaka 57 iliyopita.

Gareth-Bale-e1441344978924

Hii ni baada ya kupata ushindi wa dakika za lala salama wa goli 1-0 wakati ikicheza na Cyprus jana kwenye mechi ya kuwania kufuzu kucheza michuano ya Ulaya mwaka 2016.

2BF36B4B00000578-3221422-image-a-18_1441344444202

Shujaa wa mechi hiyo alikuwa ni Gareth Bale aliyefunga goli hilo kipindi cha pili kwenye dakika ya 82 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Jazz Richards na mpira kutinga moja kwa moja ndani ya nyavu za juu za Cyprus na kufungulia sherehe kwa mashabiki wa Wales waliosafiri kwenda Cyprus kuishangilia timu yao.

2BF369CF00000578-3221422-image-a-81_1441312877018

2BF376EB00000578-3221422-image-a-44_1441346377724

Hivi ndivyo msimamo ulivyo sasa

Kufuzu-Euro-1

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents