Habari

Gari ya Mboni Masimba yapata ajali


Gari la mtangazaji wa kipindi cha ‘The Mboni Show’ kinachoruka kila alhamis kupitia EATV, Mboni Masinga limepata ajali.

Hata hivyo, Mboni aliyekuwemo kwenye gari hilo na dereva wake hawakujeruhiwa.

Alfajiri ya leo jumapili kupitia blog yake kumeandikwa habari yenye kichwa cha habari kisemacho, “GARI la Mboni wa “The Mboni Show” lapata ajali mbaya jijini Dar es Salaam.”

Katika habari hiyo kunaonekana gari ya Mboni yenye rangi nyekundu ikiwa imeharibika mbele.

“Mboni pamoja na dereva wake ni wazima, tunashukuru Mungu. Asanteni sana kwa pole zenu wadau wangu na fans wangu wa “The Mboni Show,” ameandika Mboni kwenye blog yake.

Hata hivyo hakujatolewa ufafanuzi wa namna ajali ilivyotokea na imetokea lini japo tunahisi inaweza kuwa imetokea jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents