Michezo

Garry Neville: Baada ya kupokea kipigo cha goli 7-0 hafikirii kabisa kujiuzuru

Kocha wa Valencia Garry Neville baada ya kupata kipigo cha cha goli 7-0 kutoka kwa FC Barcelona amewaambia waandishi wa Habari kuwa hafikirii kabisa kujiuzuru na ataendelea kuwa kocha wa Valencia hadi pale mkataba wake utakapoisha.

30DA3EC800000578-0-image-m-20_1454579707532

Valencia ilifungwa goli 7-0 jana katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya mashindano ya Copa del Rey na magoli ya Barcelona yalifungwa na Luis Suarez aliyefunga magoli manne na Lionel Messi aliyefunga magoli matatu.

Valencia hadi saivi hawajashinda mchezo wowote kati ya michezo nane waliyocheza La Liga na Neville alipoulizwa kuhusu mustakabali wake katika timu alijibu kifupi “hapana” alipoulizwa kama anahofu ya kufukuzwa alijibu “swali linalofuata”.

“Ilikuwa ni moja ya matokeo mabaya kuwahi kutokea katika maisha yangu ya soka kama mchezaji lakini pia kama meneja, Tulifanya makosa mengi sana ambayo huwezi ukayafanya dhidi ya timu kama hii’, Alisema Garry Neville.

Valencia watakuwa na kazi nzito ya kuifunga Fc Barcelona magoli 8-0 katika nusu fainali ya pili ili kutinga fainali ya Copa Del Rey.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents