Michezo

Gary Neville ateuliwa kuwa kocha mpya wa Valencia ataungana na ndugu yake Phil Neville

Beki wa zamani wa kulia wa Manchester United na Uingereza Gary Neville ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Valencia hadi mwisho wa msimu.

2EFCC2A800000578-3343348-image-a-29_1449088463103

Neville, 40, ataanza rasmi majukumu yake kamili Jumapili, na atasalia kwenye benchi la wakufunzi la Uingereza. Peter Lim, mmiliki wa Valencia anayetoka Singapore, ana hisa katika klabu ya Salford City, ambayo Neville ni mmiliki mwenza.

2EFCDFB900000578-3343348-image-a-28_1449088453935

Kaka yake Neville, Phil, aliyejiunga na klabu hiyo ya Uhispania kama meneja msaidizi Julai atasalia kwenye benchi la wakufunzi.

2F0039E200000578-0-image-a-45_1449092383829

“Nimefurahia sana kupewa fursa hii,” amesema Neville. “Valencia ni klabu kubwa – na najua kujitolea kwa mashabiki wake, kutoka kwa wakati wangu nikiwa mchezaji.”

Mechi ya Jumatano ligi ya klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Lyon itakuwa ya kwanza kwa Neville akiwa kwenye usukani.

Neville amechukua nafasi ya Nuno Espirito Santo, aliyejiuzulu baada ya Valencia kuchapwa 1-0 ugenini Sevilla. Klabu hiyo kwa sasa ipo nambari tisa kwenye ligi ya Uhispania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents