George Bush apata Mkwe!

Ilikuwa ni bonge ya pati ndani ya kjiji cha Crawford katika jimbo la Texas, Marekani jumapili hii ambapo Jenna Bush, 26, mtoto wa rais George W. Bush wa Marekani alivyofunga ndoa na Henry Hager, 30

Harusi ya Jenna Bush
Jenna Bush na Henry Hager


 


Ilikuwa ni bonge ya pati ndani ya kjiji cha Crawford katika jimbo la Texas, Marekani jumapili hii ambapo Jenna Bush, 26, mtoto wa rais George W. Bush wa Marekani alivyofunga ndoa na Henry Hager, 30.


 


Harusi ya Jenna Bush


 


Walishuka ndani ya Airforce One huku Bush akiwa amemshika mkono binti yake tayari kabisa kwenda kumkabidhi kwa mume wake mtarajiwa na pembeni akiwa Laura Bush,mama wa mzazi wa bibi harusi. Moja kwa moja mpaka kwenye sehemu maalumu iliyoandaliwa kwa maharusi hao,ambapo ibada inachukua nafasi yake maalumu inajulikana kama altare na kumkabidhi kwa bwana harusi.


 


Harusi ya Jenna Bush
Rais wa Marekani George Bush pamoja na mkewe na watoto wake


 


Siku hiyo ya harusi iliudhuriwa na watu mbalimbali maarufu na viongozi wa nchi hiyo hivyo kuongeza idadi ya watu.


 


“Mtoto wetu Jenna ameolewa na mwanaume ambaye naamini atakuwa mwema kwake kwani anaonekana ni mtu safi kabisa,tunawaombea barka zote waweze kuishi maisha ya furaha”aliyasema hayo kwa waandishi wa habari akielekea kupanda pipa kurudu Washington D.C mara baada ya sherehe za harusi hiyo.


 


Harusi ya Jenna Bush


 


Bush alijistukia kuwa sio msemaji mkuu wa siku hiyo lakini alisema inabidi aongee kwani siku hiyo ilikuwa maalumu saa kwake na kwa familia yake kwa ujumla. Kwa upande wa msemaji wa bwana harusi hakuweza kusema lolote zaidi ya kushukuru harusi hiyo kufanyika kwa usalama na kuwaombea maisha mema maharusi hao.


 


Pacha wa bibi harusi na msimamizi wa bibi harusi walisoma risala maalumu iliyoandaliwa kwa Bwana na Bibi Huger. Sherehe hiyo ilifana na mara baada ya kumaliza kwa shamrashamra hizo maharusi hao waliondooka kuelekea kwenye honey mooon yao huku Bush na familia yake wakirudi jijini DC.


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents