Michezo

George Lwandamina aungana na Yanga SC kuikabili Welayta Dicha ya Ethiopia

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, George Lwandamina ameungana na timu yake hiyo ya zamani kwa kuandika ujumbe unaoitaka kuhakikisha inachomoza na ushindi dhidi ya wapinzani wao Welayta Dicha kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika unaotarajiwa kupigwa hii leo majira ya saa 10:00 alasiri.

Yametimia, George Lwandamina aitosa Yanga SC ajiunga rasmi na Zesco United

Katika kuonyesha mapenzi yake kwa wanajangwani hao na bado yupo pamoja nao, Lwandamina ameamua kuungana na Yanga SC kwenye kipindi hiki kwa kuandika ujumbe huo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Facebook.

Ushindi ni fikra inayofurahisha nafsi ya kila kitu. Kila lakheri vijana.

Lwandamina akosekana benchi la ufundi, kikosi kamili cha Yanga SC vs Singida United hiki hapa

Lwandamina ameandika maneno hayo ambayo yatakayo leta faraja kwa mashabiki na wachezaji wa Yanga SC na hamasa wakati wakiwa wanakabiliwa na mechi dhidi ya Welayta Dicha michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents