Michezo

George Zimmerman na rapper DMX kuzichapa ulingoni, ni katika pambano la raundi 3

Mtu aliyetuhumiwa kuhusika na mauaji ya Mmarekani mwenye asili ya Afrika, Trayvon Martin, mwaka 2012, George Zimmerman, aliyeachiwa huru mwaka jana, atazichapa na rapper DMX kwenye pambano la ndondi la raundi 3, imefahamika.

george-zimmerman-prosecutors-messed-up-the-first-week-of-his-second-degree-murder-trial
George Zimmerman

Zimmerman ndiye aliyependekeza kuwa na pambano la ngumi na staa yeyote.

Pambano hilo limeandaliwa na promoter maarufu, Damon Feldman wa kampuni ya Celebrity Boxing. Wiki iliyopita alisema alikuwa anakubali ombi la mtu yeyote atakayependa kupanda ulingoni kupambana na Zimmerman katika pambano litakalooneshwa kwa kulipia.

“Habari hiyo ina saa moja tu e-mail yangu imejaa zaidi ya watu 8,000 wanaotaka kuchuana na George, ” Feldman aliiambia CNN wiki iliyopita.

Mapema Jumatano hii amesema amemchagua mshindani. Katika maombi zaidi 15,000 yaliyotumwa kwa e-mail, amesema amemchagua DMX. Tarehe, muda na sehemu ya pambano hilo itatangaza Jumatano ijayo.

DMX
DMX

“I am going to beat the living f**k out him … I am breaking every rule in boxing to make sure I f**k him right up,” DMX aliuambia mtandao wa TMZ.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents