DStv Inogilee!

Georgina Rodriguez amwaga machozi hadharani baada ya kumshuhudia mpenzi wake, Ronaldo akifunga ‘hat-trick’ dhidi ya Atletico

Mchezaji bora kabisa duniani, Cristiano Ronaldo amemfanya mpenzi wake, Georgina Rodriguez kumwaga machozi ya furaha hadharani baada ya kushuhudia akifungia mabao matatu ‘hat-trick’ timu yake ya Juventus dhidi ya Atletico Madrid usiku wa siku ya Jumanne na kuiwezesha kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya mabingwa barani Ulaya.

Mreno huyo ameweza kupindua matokeo kwa kufunga 3 – 0 na kuwafanya wengi kubaki vinywa wazi kwakuwa waliamini Juve inakamilisha ratiba kutokana na kukubali kipigo cha mabao mawili kwa bila kwenye mechi ya kwanza iliyopigwa jijini Madrid nchini Hispania.

Cristiano Ronaldo's girlfriend Georgina Rodriguez cries tears of joy on Tuesday evening

Georgina Rodriguez ambaye ni mama wa watoto mapacha aliyozaa na nyota huyo aliyewahi kuwa mchezaji wa Real Madri, alijikuta akishindwa kuyazuia machozi yaliyokuwa yakimtoka baada ya kumuna mpenzi wake akiisaidia timu yake ya Juventus kuingia hatua ya robo fainali.

Ronaldo's son, Cristiano Junior, punches the air after watching his dad make it 3-0 on the night

Mtoto wa Ronaldo, Cristiano Junior, akishangalia baada ya bao la tatu alilotupia baba yake 3-0

Katika mchezo huo uliyokuwa muhimu kwa wenyeji Juvuntus, Ronaldo aliibeba familia yake ambayo ni mpenzi wake pamoja na mtoto wake wa kiume Cristiano Junior kushuhudia mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Allianz Stadium. 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW