Michezo

Gerard Pique aonja joto la jiwe

Beki wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Gerard Pique hapo jana usiku alipata msukosuko kutoka kwa mashabiki baada ya kuzomewa wakati wa mchezo wao dhidi ya Albania wa kuwania tiketi ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2018.

Kabla ya mchezo huo Pique alisema kamwe hawezi kuondolewa katika timu ya taifa kwa sababu ya kuunga mkono waliyokuwa wanahitaji wa Catalonia kujitenga na Hispania.

Pique ameonysha msimamo wake wazi kuhusu Calatonia kujitenga na Hispania, jambo ambalo linaonekana kuwaudhi wengi wasiopenda mgawanyiko huo.

Katika mchezo huo timu ya taifa ya Hispania ilichomoza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Albania hivyo kujihakikishia kufuzu kombe la dunia kwa kuongoza kundi G kwa kuwa na jumla ya pointi 25.

Pique, mwenye umri wa miaka 30, ataukosa mchezo wa mwisho siku ya Jumatatu huko Israel kufuatia adhabu aliyopewa baada ya kumsukuma mchezaji Armando Sadiku katika kipindi cha pili, mabao ya timu hiyo yamefungwa na wachezaji Rodrigo, Isco na Thiago.

Sio mashabiki wote waliyokuwa wakimzomea bali wapo wengine ambao walikuwa  wakimuunga mkono na kuandika “Gerard Pique wewe ni bora tunahitaji fulana yako.”

Kwa matokeo hayo unaifanya timu ya taifa ya Itali ambayo imetoka sare ya bao 1-1 na Macedonia kupata nafasi ya moja kwa moja kushiriki michuano hiyo huku wakiwa na pointi 20 nyuma Hispania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents