Michezo

Gervinho aihama As Roma ajiunga na timu ya Hebei China Fortune FC

Klabu ya AS Roma ime muuza rasmi mchezaji wake Gervinho kwenda Hebei China Fortune FC kwa ada ya €18m pamoja na bonus ya €1m.

Gervinho-Hebei

Mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast alipigwa picha akiwa ameshikilia jezi ya klabu yake mpya ambayo ataitumikia lakini mambo mengine ya kimkataba yamefanyika Feb 28.

“Raiya huyo wa Ivory Coast mwenye miaka 28 amesaini mkatba na klabu hiyo ya China kwa mkataba wa kudumu wenye thamani ya €18 million baada ya kudumu na AS Roma kwa misimu miwili na nusu”.

“Nyongeza ya €1 million italipwa kutegemea na kiwango cha mchezaji huyo atakacho kionyesha katika klabu hiyo ya China”.

Gervinho alijiunga na Roma majira ya joto ya mwaka 2013 akitokea Arsenal.

Gervinho amecheza michezo 88 kwenye mashindano yote akiwa anaitumikia Roma na kufunga magoli 26. Amefunga magoli saba kwenye mechi 17 msimu huu.

Mechi yake ya mwisho akiwa Roma ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Milan mchezo uliochezwa January 9, 2016.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents