Ghala la Silaha lalipuka Mbagala

Leo asubuhi ghala la silaha la Jeshi limelipuka katika kambi ya Jeshi iliyoko Mbagala Kizuiani na kutikisa jiji zima, serikali imetoa tangazo kwamba watu wote mjini washuke maghorofani.

Polisi, zimamoto pamoja na wanajeshi wanajitahidi kuzima moto mkali uanoendelea kuteketea na kusababisha mabomu mengine kulipuka, lakini inasemekana kwamba moto huo utaweza kuzimika kwa utaalamu wa hali ya juu na siyo kwa njia za kawaida.

Usalama katika eneo la kambi ni ndogo na wakazi wengi wa Mbagala wameondolewa.

Inasemekana kuwa waliyojeruhiwa ni zaidi ya mia, tutawaletea picha na habari zaidi baada ya muda mfupi…

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents