Habari

Ghana kuongeza umri wa wasichana kuolewa kutoka 18 hadi 23

Wakati Kenya ikiwa imewasilisha bungeni muswaada wa sheria ya ndoa 2013 Jumanne ya wiki hii, kuna uwezekano wa nchi ya Ghana kuongeza umri wa wasichana wa nchi hiyo kuolewa kutoka 18 wa sasa hadi 23.

rings-3

Mapendekezo hayo yametolewa na mtakwimu Mkuu wa serikali ya Ghana, Bi Philomena Nyarko, ambaye amesema hatua hiyo itawafanya wanawake kujiandaa vyema kiakili na kimwili kuzaa watoto, na kwamba, itapunguza ongezeko la idadi ya watu nchini Ghana kwa kati ya 15% hadi 20%.

Bi Nyarko amesema, wanawake wanaochelewa kuolewa ama kuzaa hadi umri wa miaka 23 wanakuwa na afya njema.
“Inafahamika vizuri kwamba, matokeo ya afya njema kwa mama na mtoto, endapo atachelewa kuzaa hadi msichana anapokuwa amekomaa vya kutosha kwa ajili ya kuolewa na kubeba mimba ili kuokoa maisha ya mama na mtoto”, amesema Bi. Nyarko.

Mapendekezo hayo yamekuja kipindi ambacho wabunge nchini Nigeria wanajadili kuhusu kupunguza umri wa kuolewa kutoka miaka 18 ya sasa ili watu waweze kuoa na kuolewa katika umri mdogo zaidi.

SOURCE: BBC SWAHILI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents