Habari

Ghana: Msitu uliyopo chini ya maji mbao zake kutumika kujenga upya kanisa lililoungua moto Paris

Mbao aina tofauti kutoka msitu wa chini ya maji nchini Ghana huenda ikatumika kujenga upya kanisa kongwe la Notre-Dame baada ya paa lake lake kuchomeka mwezi Aprili.

Scene of blaze in Paris

Msitu mkubwa wa tropiki umekua ukikuzwa chini ya ziwa Volta tangu mwaka 1965, baada ya ujenzi wa bwala la Akosombo nchini Ghana kusomba sehemu ya ziwa Volta.

Kampuni moja ya Ghana, iliyopewa zabuni ya kuvuna mbao hizo, inaamini kutumia mbao hizo kujenga upya Notre-Dame ni njia rafiki kwa mazingira badala ya kukata miti.

Ziwa Volta inaukubwa wa mita 3,300 mraba

Ziwa Volta inaukubwa wa mita 3,300 mraba

Kete Krachi inasema mbao hizo ni “imara zaidi” kwa sababu imehifadhiwa kwa njia ambayo haiwezi kuozeshwa na hali yoyote ya mazingira ya ziwa hilo.

Huku baadhi ya wataalamu wakielezea pendekezo hilo kama ”mbinu muafaka”, wengine wanaonya mbinu hiyo huenda ikaathiri mfumo wa ikolojia.

Kampuni hiyo imewasilisha pendekezo lake kwa serikali ya Ufaransa, ikitilia mkazo kwamba kutumia mbao kutoka ziwa Volta kutasaidia kurejeshea Notre-Dame muundo wake asilia.Picha za Notre-Dame Cathedral mwezi Juni 2019.Paa la Notre-Dame na mnara wake ilivunzika baada ya moto kuteketeza sehemo ya kanisa hilomwezi Aprili

Inakadiriwa karibu miti 1,300 ya aina ya mwaloni (oaks) ilitumika katika karne ya 12 kujenga fremu na mnara wa jengo la zamani la Notre-Dame.

Msitu wa ekari 52 ulioharibiwa wakati huo- ambao ni sawa na viwanja 26 vya mpira.

Kwa mujibu wa Bertrand de Feydeau, naibu rais wa kundi la uhifadhi la du Patrimoine, anasemaUfaransa halina miti mikubwa ya mwaloni kama ile iliyotumika kwa ujenzi wa jengo la kwanza asilia.

Francis Kalitsi, mwenyekiti na mwanzilishi wa Kete Krachi, anaunga mkono wazo hilo. ”Sidhani wana miti ya mwaloni kwa kiwango kilichotumiwa kujenga kanisa hilo,” alisema.

Kete Krachi tayari inakata miti ya mbao kutoka chini ya maji kwa kutumia mashini inayotumia video, sonar na mfumo wa GPS.

Baadhi ya mbao hizo zinasafirishw ana kuuzwa katika mataifa ya Ulaya na zingine nchini Africa Kusini, Asia na mashariki ya kati.Kete Krachi inatumia mashini maalumkukata mbao kutoka ziwa Volta.Jinsi mbao zinavyotolewa katika Ziwa Volta kwa kutumia mashini maalum

Kampuni hiyo inasema ikipewa jukumu la kukarabati kanisa hilo, itauzia serikali ya Ufaransa mbao za thamani ya dola milioni $50m sawa na (£39.5m).

Pendekezo lake tayari limeidhinishwa na wizara ya utamaduni.

Jérémie Patrier-Leitus kutoka wizara ya utamaduni ya Ufaransa ameiambia BBC: “Kufikia sasa hatujabaini fremu ya jengo hilo itajengwa upya kwa kutumia mbao. Tuko katika mchakato wa kuhifadhi jengo hilo kwanza kisha tuanze shughuli ya ujenzi wa paa na mnara wa jengo hilo.

“Ujenzi mpya wa kanisa hilo konge utaanza baada kuta zake kuimarishwa. Tunatathmini mapendekezo kadhaa yaliowasilishwa ili kuthibitisha vifaa vilivyotumiwa kujenga fremu hizo.”

Bog oak: Mbao thabiti zaidi

Dkt Cathy Oakes, mtaalmu wa uchoraji ramani ya nchumba kwa kifaransa na Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Oxford, amesema mbao kutoka ziwa Volta huenda inafanana na “bog oak”, amabyo inatumika sana kuchonga fanicha lakini sio Notre-Dame asilia.

“Bog oak imekua ndani ya maji kwa muda mrefu , kwa hivyo ni imara na inadumu kwamuda mrefu” alisema katika warsha moja kabla ya kifo chake.Mbao inayopatikana chini ya Ziwa Volta huenda ikaimarisha sekta ya mbao ya GhanaMbao inayopatikana chini ya Ziwa Volta huenda ikaimarisha sekta ya mbao ya Ghana

Lakini hatua hii itakua na athari gani kwa mazingira?

Wataalamu wa mazingira wanahofia hatua ya ukataji miti chini ya ziwa Volta huenda kukaathiri mfumo wa ikolojia.

Ripoti iliyochapishwa katika jarida la ubora wa mazingira maarufu Environmental Health Perspectives ilisema kukata miti kutoka chini ya maji kunaharibu mazingira ya chini ya maji kwa kuziba mwanga unaotumiwa na viumbe majini.Miti iliyokatwa chini ya maji ikipakiwa kwenye chombo cha majini kupelekwa katika kiwanda cha mbao

Miti iliyokatwa chini ya maji ikipakiwa kwenye chombo cha majini kupelekwa katika kiwanda cha mbao

Miti hiyo pia hutoa makazi kwa samaki na wanyama wengine wa porini. Kuikata huenda kukaathiri mfumo wa ikolojia ziwani, hali ambayo pia inatishia sekta ya uvuvi nchini Ghana – ambayo inategemewa na karibu familia 300,000.

Stephen Anani, afisa wa mradi unaoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali linalojulikana kama Rafiki wa Taifa, ameimmbia BBC kwamba ukataji wa miti chini ya maji that removing ulichangia “kupungua sana” kwa idadi ya samaki katika ziwa Volta kwasababu wanazaana kando kando ya matagaa ya miti hiyo.Miti iliyokatwa kutoka chini ya ziwa Volta

Miti iliyokatwa kutoka chini ya ziwa Volta

“Itaharibu makazi asilia ya samaki na pale wanapotagia mayai yao,” alisema. “Baadjhi ya wavuvi wanahofia kazi yao itaathirika. Ukizungiumza na wavuvi wanaoendesha shughuli zao katika ziwa hilo wanalalamika kwa machungu.”

Kampuni ya mbao ya Kete Krachi inasisitiza kuwa haing’oi miti, bali inakata semu ya juu, na kwamba haifikii mizizi yake . Inasema hatua hiyo “inapunguza” hatari ya kuharibu mfumo wa ikolojia.

Maswali pia yameulizwa kuhusu uchafuzi wa mazingira unaotokana na ukataji miti hiyo na kuisafirisha kutoka Ghana hadi France.Timber from Lake Volta stacked up before it is cut in a saw mill.

Timber from Lake Volta includes typical African hardwoods such as iroko and wawa

Dkt John Recha, mwanasayansi na mtafiti wa kimataifa wa masuala ya kilimo mwenye makao yake mjini Nairobi, anasema ukataji wa miti ya mao na usafirishaji wake hadi nchini Ufaransa kutaacha msururu “mkubwa” wa hewa chafu.

“Meli hutumia mafuta mengi,” aliimbia BBC. “Mashini inayotumiwa baharini na ziwani inahitajimafuta mengi, ambayo hutua gesi chafu hewani inapotumika.”Wavuvi wakijianda kwanda kuvua samaki mjini Accra.

Badhi ya wavuvi wanahofia kukata miti chini ya ziwa Volta huenda kukapunguza idadi ya samaki

Kete Krachi inashikilia kuwa viwango vya uchafuzi wa hewa kutokana na ukataji wa miti kutoka chini ya maji viko “chini sana” ikilinganishwa na ukataji wa miti ardhini.

“Kiwango kikubwa cha mafuta hutumiwa kusafiricha mbao – pia usafiri wa majini ni wa gharama nafuu ukilinganishwa na uasafiri wa ardhini ,” Bw. Kalitsi alisema.

Maelezo kuhusu Notre-Dame

Kanisa hilo hupokea karibu wageni milioni 13 kila mwaka, idadi ambao ni kubwa kuliko watalii wanaozuru Eiffel Tower

Lilijengwa katika karne ya 12 na 13 na limekuwa likifanyiwa ukarabati mkubwa. Sanamu kadhaa ziliondolewa kanisani hapo ili kuruhusu ukarabati wake.

Palaa la lanisa hilo lililoteketezwa na moto lilikua limetengenezwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mbao Dkt Tristan Smith, ni mtaalamu wa kusafirisha mizigo mjini kutoka Chuo Kikuu cha kawa cha London, anakubali kuwa usafirishaji mizigo kwa kutumia bahari inasadikiwa kuwa njia salama zaidi ya usafiri linapokuja suala la kuhifadhi mazingira.Mbao inayotokana na miti iliyomea chini ya maji inasemekana kuwa thabiti zaidi inapotumiwa kwa ujenzi

Mbao inayotokana na miti iliyomea chini ya maji inasemekana kuwa thabiti zaidi inapotumiwa kwa ujenzi

Hatahivyo ameonya kuwa uchafuzi wa mazingira kutokana na usafiri haujadhibitiwa kama viwanda vingine, hivyo basi mpango wa kusafirisha mbao hizo huendaisiwe rafiki kwa mazingira kama inavyodhaniwa.

Kete Krachi inase,a meli inayopanga kutumia itasafiri Ufaransa kung’amua njia ya biashara ili kutathmini kiwango cha hewa ya caboni itakayoachilia hewani.Mashini ya Kete Krachi'inayotumiwa kukata mbao kutoka Ziwa Volta.

Kusafirisha bidhaa kwa kutumia usafiri wa majini kunaweza kusaidia kuhifadhi mafuta kuliko usafiri wa ardhini

Kampuni hiyo inaamini kuhusishwa kwake kujenga upya kanisa la Notre-Dame hakutakua na manufaa ya kiuchimi pekee kwa Ghana, lakini pia itakua na umuhimu mkubwa kihistoria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents