Ghana: Waitoa Afrika Kimasomaso

Timu ya Ghana baada ya kutua robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2010 kwa kishindo huko Afrika ya Kusini,sasa wanajiandaa kukutana na timu ya Uruguay,ambao wadau wengi wanaipa nafasi hata kulitwaa kombe la dunia kutokana na makali ya ball wanaloonyesha.

Kwa Upande mwingine timu ya Black Stars kutoka Ghana inaongozwa na wachezaji wenye Umri mdogo kama Kevin Prince Boateng ,Asamoah Gyan,Didier Ayew na Antony Anaan,wanaonyesha nguvu nyingi ya kuinyanyua timu hiyo.

Anaan ambaye ndiye mchezaji aliyechukua nafasi ya Micheal Essien nyota ambaye ni majeruhi kwa msimu huu wa World Cup 2010,ameonyesha ustadi wa soka kiasi cha club tofauti Ulaya kumtolea macho kana kwamba ndiye nyota anayemfuatia Essien.

Ghana ina mtihani mgumu wanapokutana na Uruguay wiki hii lakini wengi wanaamini,wakiendelea kuonyesha makali kama yale tuliyoshuhudia kati yao na USA, Ghana itafika mbali katika michuano hii.

Kocha wa Ghana,Milovan Rajevac amesema timu yake ili stahili ushindi dhidi ya USA kwani mchezo ulikuwa mzuri kiasi cha kuwashangaza mashabiki na dunia.

Akizungumzia mechi inayokuja ya Uruguay,amesema ingawa wapinzani wao ni wakali,Ghana itajiandaa na ina kila sababu ya kushinda.

Mungu ibariki Ghana. Mungu Ibariki Afrika

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents