Burudani

Gharama ya ndinga mpya ya Drake ni sawa na kurudia uchaguzi zaidi ya majimbo 10

Rapper kutoka Canada, Drake ameonyesha kuwa yeye ni moja ya watu walio na love ya kutosha na magari kwa kuamua kuvuta ndinga nyingine ambayo gharama yake ni sawa na gharama ya kurudia uchaguzi kwa majimbo zaidi ya kumi nchini Tanzania.
Gharama ya ndinga hiyo aina ya ‘Ferrari LaFerrari  kutoka kwa hitmaker wa ‘God Plan’  ni kiasi cha dola milioni saba sawa na kiasi cha shilingi  bilioni tano na ushehe za Kitanzania (15,753,827,457.68)

Kwa mujibu wa ripoti inaeleza pia kuwa rapper huyo anamiliki gari aina ya Bugatti Veyron, yenye thamani ya kiasi cha dola milioni mbili, tolea la mwaka 2010 aina ya Sang Noir pia ana gari kama Bentley Continental GTC, S-Class coupe-, Lamborghini Aventador Roadster na Rolls Royce Phantom vile ana McLaren 675LT pamoja na gari aina ya Mercedes-Benz .

Kwa idadi hiyo mpaka sasa Drake ana jumla ya gari zisizopungua saba nyumbani kwake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents