Burudani

Ghetto Kids wamneemesha Eddy Kenzo kupitia video ya French Montana ‘Unforgettable’

Hitmaker wa Sitya Loss, Eddy Kenzo alisaini makubaliano na star wa Marekani, French Montana ili madancer wake ambao ni watoto walio chini ya uangalizi wake, wanaojulikana kama Ghetto Kids waweze kucheza kwenye video ya wimbo mpya ya rapper huyo aliomshirikisha Swae Lee wa kundi la Rae Sremmard, Unforgettable.

Video hiyo imefanyika nchini Uganda.

Akiongea na Nemmy Kim wa Mlimani Radio, Kenzo amesema alipata dili hilo baada ya French Montana kuona video ya wimbo wake, Sitya Loss na kuvutiwa na uchezaji wa watoto hao.

Ilimlazimu Montana kupitia mtandao wa YouTube kuwafuatilia zaidi Ghetto Kids na kuonesha kuvutiwa nao kiasi cha kuamua kuwafuata Uganda kwaajili ya kufanya nao kazi.

Naye French Montana kupitia Instagram aliwahi kuelezea jinsi alivyowafahamu Ghetto Kids.

I was on YouTube listening to music from one of my favorite African artists Cheb Hasni and found this video of these kids dancing barefoot in the mud and on rocks. No complaining or pain just so much joy in the music and dancing. I watched with “Unforgettable” playing in the background and it hit me! Their moves went to the tempo and it was almost like God planned it! It inspired me to go find them in Uganda. My team and I searched and we found them. When we arrived, it was so sad for me to find out that one of the kids in the video died before I got to meet him, and my favorite girl Patricia had just woken up from a 2 week coma. But it did not stop her from coming to the set and dancing barefooted with the others. These kids made my experience in Uganda

Imeandikwa na Nemmy Kim (Mlimani Radio)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents