Michezo

Gianni Infantino awa Rais mpya wa FIFA

Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA jana Ijumaa ya February 26 ndio siku lilifanya uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais wa kuziba pengo la Sepp Blatter. Katibu Mkuu wa zamani wa UEFA, Gianni Infantino amekuwa Rais mpya wa FIFA, baada ya kumshinda Sheik Salman.

3196ED7700000578-3465464-image-a-17_1456506927996
Rais mpya wa FIFA Gianni Infantino

Gianni Infantino alishinda katika raundi ya pili ya uchaguzi baada ya kurudiwa nafasi hiyo ya Urais kwa jumla ya kura 115, na kumzidi mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa kwa zaidi ya kura 27, wakati Prince Ali bin al-Hussein akishika nafasi ya tatu kwa kuwa na kura nne.

Infantino amabaye ana miaka 45 ni mwanasheria kitaaluma anatokea Valais maili chache kutoka makazi ya Sepp Blatter yalipo.

Amekuwa Rais wa tisa wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika mjini Zurich, Uswisi na akaahidi kurejesha hadhi ya soka uliwenguni katika zama mpya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents