Kundi la muziki la Gidi Gidi Maji Maji lenye maskani yake nchini Kenya na kufanyia shughuli zake za kimuziki kule Cape Town, Afrika Kusini litakuwa ni kundi la kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kutumbuiza kwenye tamasha kubwa la Reggae linalokwenda kwa jina la Reggae on the River Festival. |
Story by: Daniel Nyalusi
Kundi la muziki la Gidi Gidi Maji Maji lenye maskani yake nchini Kenya na kufanyia shughuli zake za kimuziki kule Cape Town, Afrika Kusini litakuwa ni kundi la kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kutumbuiza kwenye tamasha kubwa la Reggae linalokwenda kwa jina la Reggae on the River Festival.
Tamasha hilo litafanyika mwezi ujao nchini Marekani kwenye Jimbo la California ambalo litahudhuriwa na wasanii wakubwa kwenye Muziki wa Reggae, Ragga na Dancehall.
Wakiongea kwa simu kutoka Afrika Kusini wasanii hao wamesema wamepata nafasi ya kuperform na kuonesha uwezo wao mbele ya wasanii wakubwa kama Sean Paul, Sizzla, Israel Vibration, Ziggy Marley, Anthony B na wengine kibao kutoka Jamaica na Ulaya.
Msemaji wa kampuni inayoandaa Judy Mowatt alisema Gidi Gidi Maji Maji hawatakuwa peke yao kutoka Afrika bali watashirikiana na Knaan msanii wa kisomali anayetamba katika Muziki huko majuu na anayefanya shughuli zake za kisanii nchini Canada na Salif Keita kutoka nchini Mali.
Source: Bongo5