Burudani ya Michezo Live

Giroud adai Mungu amehitaji abaki Chelsea

Olivier Giroud anaamini Mungu amemuhitaji yeye aendelee kubaki Chelsea baada ya striker huyo kuongeza kandarasi ya kusalia the Blues.

The 33-year-old was rewarded with a contract extension until the end of next season

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 watu wengi walitarajia angeondoka Stamford Bridge mwezi Januari ili kupata nafasi ya kucheza zaidi itakayomsaidia kuendelea kuitumikia timu yake ya taifa inayonolewa na Didier Deschamps katika michuano ya Euro 2020.

Lakini, Giroud aliwashangaza wengi baada ya kutokea benchi kwwenye mchezo wa Premier League dhidi ya Manchester United.

Chelsea striker Olivier Giroud (centre) was in high spirits at training on Wednesday

Giroud kisha akaja kuanza kwenye michezo mitano iliyofuata ya Frank Lampard huku akifunga goli kwenye ushindi wa mechi ya nyumbani dhidi ya Tottenham na Everton kabla ya Premier League kusimamishwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

Na kupelekea, Giroud kuongezewa mkataba ambao utamfanya kuendelea kusalia Stamford Bridge hadi mwisho wa msimu ujao.

”Nilipaswa kuondoka dirisha la mwezi Januari, kwa sababu sikucheza vyakutosha nilihitaji michezo zaidi ili kuwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano ya Euro 2020,” amesema Giroud.Giroud was keen to repay the faith of boss Frank Lampard after he was given more game time

”Ilikuwa bado kidogo tu mimi kuondoka ndani ya klabu lakini hakika nafikiri Mungu alihitaji mimi niendelee kuwa hapa Chelsea. Kocha aliniambia kuwa asingeliweza kuniacha niondoke kwasababu hakuwa na mtu yoyote wa kuchukua nafasi yangu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW