Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Global Publishers yazindua msimu mpya wa kushinda pikipiki

Kampuni ya Global Publishers itaanza kuendesha shindano maalum kwa ajili ya wasomaji wake ambao watajishindia pikipiki ambazo kila wiki itatoka moja.

Wasomaji wa Magazeti ya Michezo ya Championi, yanayotoka siku nne kwa wiki, yani Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi pamoja na Spoti Xtra linalotoka kila Jumapili pamoja na Magazeti Pendwa ya Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani na Uwazi, watafaidika.

Pikipiki 12, zimetengwa kwa ajili ya wasomaji hao ambapo kila wiki itatoka moja pamoja na zawadi zingine za simu, fulana, ada ya shule na vyombo vya ndani.

Pia Global Publishers inapenda kuwataarifu wasomaji wake kuwa, gazeti moja litatumika kwa SMS moja tu na siyo vinginevyo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW