Burudani

Go Hellen! Go Tanzania!

 

Hellen Dausen, mwakilishi wa Tanzania Katika Miss Universe 2010, anatarajia kupanda stejini usiku wa leo kuwania taji la Miss Universe 2010, ambalo linasadikika kuwa kubwa zaidi ya yote katika ulimwengu wa urembo Duniani.

Mrembo huyo anatarajia kuchuana na Warembo zaidi ya mia moja kutoka nchi mbalimbali Duniani.

Mratibu wa Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi amempa nafasi kubwa sana mshiriki huyo kwani anamvuto na haiba kuliko wenzake wengi katika kambi hiyo iliyopo katika Hoteli ya Mandalay Bay Resort mjini Las Vegas Nchini Marekani.

Maria na Hellen wote wanawasihi waTanzania kupiga kura ili kumzidishia nafasi za ushindi mrembo huyo pamoja na kupeperusha Bendera ya Tanzania juu zaidi.

Tunamtakia Kila la Kheri Usiku wa Leo.

Go Hellen!

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents