Burudani

Godzilla achomoa kauli ya Daxco Chali kuhusu kutemwa MJ Records

Msanii wa Hip Hop Bongo, Godzilla amekanusha kauli iliyotolewa na Producer kutoka MJ Records, Daxo Chali kuwa ametimuliwa kutokana na kushindwa kufanya baadhi ya mambo waliokubaliana baada ya kutoa ngoma ya X.

Kipitia ENewz ya EATV, Zilla amedai kuwa hajatimuliwa MJ kama inavyodaiwa na Daxo  na yeye kufanya kazi katika studio zingine ni kutafuta flavour tofauti kwenye muziki.

“MJ ni marafiki pia mimi na Marco ni marafiki sana ila kwenye maisha lazima uongeze upana. MJ nina ngoma nyingi sana na hazijatoka coz niko busy sana kurekebisha studio za Salasala ili wana watoke,” amesema Zilla.

Aliongeza “Nina ngoma nyingi store amefanya Marco ambazo hatujazitoa zingine zilitakiwa ziwe zangu so ikabidi ziwe zake nimeziacha tu apige coz naye amazipenda, nafanya kazi muda wote na Marco ukiangalia production zingine ni addition tu kupata different flavour .”

“Daxo hawezi kudanganya na napenda anavyofanya kazi kwa bidii is very good boy hawezi kunikosea nidhamu siwezi kumkosea nidhamu ni zaidi ya familia kwa jinsi tunavyoishi na is very good kid anad nice.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents