Burudani

Godzilla aongelea mixtape yake, anayemkubali kati ya Nikki Mbishi na Wakazi, Rabbit vs Octopizzo na kuhusu 50 Cent

Rapper Godzilla aka Zizi amezungumza na Bongo5 kuhusiana na maendeleo ya mixtape yake ya Zillax, anayemkubali zaidi kati ya Wakazi na Nikki Mbishi na sababu za kupotea kwa role model wake, Curtis Jackson aka 50 Cent na mengine.

Godzilla akichana.

Kuhusu mixtape a Zillax

Mixtape inaendela vizuri. Mtu ukikaa labda Twitter au wapi wanamention ngoma zilizopo kwenye mixtape hiyo inamaanisha kuwa imewafikia na wameisikia so it’s all good inaenda vizuri.

Kuhusu yupi ni rapper mkali kati ya Wakazi na Nikki Mbishi

Mimi kwangu mkali.. Nikki mkali. Naappreaciate wote kazi zao lakini Nikki ni mkali, Nikki is crazy man. Wote ni maemcee lakini Nikki anaweza zaidi freestyle halafu za papo kwa papo halafu freestyle kama kaandika, yaani hapo ndipo wanapozidiana lakini, wote wakali lakini Nikki ana kitu cha ziada.

Kuhusu uhusiano wake na Wakazi

He is ma dawg, he is my ni*gga, one of my closest n*gga. Ni washkaji wa karibu sana.

Kuhusu yupi mkali kati ya Rabbit na Octopizzo

Itabidi nichukue time nikae vizuri.. nimesikia wote ngoma mbili tatu lakini sijaenda ile deep, I still need some time. Ila Octopizzo ana mavideo makali.

Kuhusu kupotea kwa 50 Cent

I don’t believe in that kwasababu unajua industry sometimes. Sanaa haikuweki pale unapotaka kukaa, kila mtu imemtokea kwenye muziki. Kina Hov kuna wakati hawapo wanachart akina Rozay lakini baadaye tena wanarudi. Jamaa (50) amefanya kazi nyingi sana nzuri na sasa hivi labda amewekeza muda mwingi kwenye biashara.

Kuhusu kubadilika kwenye muziki

Mimi ni msanii ambaye nafanya kila design ya muziki, I am just flexible, kama vile anavyofanya Kanye, leo yuko huku, leo hivi. Nataka nikifanya naanzishi na watu wengine wanafuata, nataka kuanzisha trend kila wakati. Ndio maana unasikia Sala Sala inasound yake, King Zilla ina sound yake, Nataka inasound yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents