Burudani

Godzilla: Ubora mdogo wa filamu za TZ unachangiwa na wingi wa makampuni ya production yasiyo na wataalam

Rapper wa Sala Sala , Dar es Salaam, Godzila amefunguka na kusema filamu filamu nyingi za kibongo zina ubora mdogo kwasababu zinatayarishwa na makampuni ya waigizaji wenyewe ambayo hawana wataalam wa kutosha kuhusu taaluma ya filamu.
GODZILLA

Akiongea na Bongo5, King Zilla ameongeza kuwa filamu za kibongo zimekosa ubora kutokana na bajeti finyu zinazotumika kuandaa filamu pamoja na kukosa wataalam wataokuwa wakifanya kazi kutokana na taaluma zao za filamu.

“Unakuta muigizaji akipata jina katika filamu tayari atafungua ofisi yake na kuanza kuzalisha filamu ambazo ameandaa yeye mwenyewe,hawajui kuna watu maalum ambao kazi zao ni kuzalisha filamu tu hizo ni kazi zao na taaluma zao zinawaruhusu kufanya kazi hiyo,hawatumii uzoefu kama wanaoutumia Watanzania katika production ya filamu zao, kwamba ukishajua kuigiza filamu basi na wewe unaweza kuwa na production yako,” alisema Godzilla ambaye ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye Fiesta ya Mtwara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents