Michezo

Goli la Neymar laipoteza Manchester United Marekani (+Video)

Mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona, Neymar Jr aameendeleza ubabe kwa kuichabanga klabu ya Manchester United goli 1-0 kwenye mchezo wa michuano ya International Champions Cup inayoendelea nchini Marekani.

Neymar akimtoka kiungo wa Man United Paul Pogba

Neymar aliipatia goli klabu yake ya Barcelona kunako dakika ya 31 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka duniani.

Kwa matokeo hayo Manchester United wamemwagwa nje ya michuano hiyo yenye msisimko zaidi kwa kipindi hiki cha mapumziko (Pre-season).

Mchezo mwingine uliopigwa ni kati ya Juventus na matajiri wa Ufaransa, PSG ambapo matajiri hao wametupwa nje ya michuano hiyo kwa kipigo cha goli 3-2.

https://youtu.be/z_JvWbzE7Gs

By Godfrey Mgallah

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents