Uncategorized

Gonga Entertainment Yawaleta Wamarekani Kuvunja Jungu


Mjasiriamali wa tasnia ya burudani Frang Gonga wa Gonga Mix Entertainment akishirikiana na Dj wa Kitanzania mwenye makazi yake huko Springfield Massachusetts nchini Marekani, wamemwalika Dj Infared Scope pamoja na msanii wake Floss kupiga shoo Tanzania wikiendi hii ambayo wao wameibatiza kama wikiendi ya Vunja Jungu.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=mrPh7DkQBGI[/youtube] Shoo itapigwa leo Ijumaa, maeneo ya Picolo beach, Kawe itakua white party na baadaye Jumapili ni Barbeque pamoja na muziki ndani ya Rudys Farm Bahari beach. Bongo5.com ilipata fursa ya kuongea na wageni hao Dj Infared Scope na msanii Floss pamoja na Mwenyeji wao Rich Maka na kusema kwamba watanzania wategemee shoo kali na nzuri kwani wao ni wachapa kazi wa kimataifa na watatoa burudani ya hatari ya nyimbo mchanganyiko kuanzia Hip Hop, R&B, Dancehall, Tecno na nyinginezo nyingi.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=LjSq6o4s1Ig[/youtube] Kwa ufupi tu Dj infared scope alianza kazi ya u Dj miaka 20 iliyopita katika jiji la New York ambapo alianza kama Dj wa House Party lakini baadae akaanzisha kundi lake la Infared Entertainment ambalo ndani yake kuna ma produsa kama God Getta and wasanii kama Floss pamoja na ma Dj wengine kama Dj Kaslay na Msanii Papoose. Akiendelea Dj Scope alisema anaona kuna mabadiliko makubwa katika upande wake kwani wakati akianza ilikuwa kupiga kwenye House Party ya watu mia mbili mia nne mpaka kupiga shoo za watu elfu kumi mpaka watu elfu 25.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=LEuykzNQkJs[/youtube] Alisema pia kuwa moja ya mafanikio yake katika u Dj ni kumiliki klabu yake mwenyewe ya usiku inayoitwa “Club O dour Night Club” iliyopo Springfields Massachusetts inayoweza kuingiza mpaka watu mia nne. Akimalizia Dj scope alisema ameshapiga shoo Ghana, Canada, Puerto Rico na sehemu nyingine nyingi.

Naye msanii Floss akiongea na Bongo5.com alisema yeye yuko chini ya Infared Entertainment ambayo inamilikiwa na Dj Scope ambapo anafanyakazi zake za kimuziki ambapo anakamilisha Mixtape Albamu yake mwezi wa 9 mwaka huu na kwamba katika kazi yake hiyo kuna uwezekano mkubwa sana msanii ama wasanii wa Kibongo ambao watakuwemo katika Mixtape hiyo.
Msanii huyo anasema yeye alizaliwa na kukulia Harlem New york na pia muziki aliuanza akiwa Jela baada ya kufungwa miaka 4 jela na ndipo ilibidi atafute njia nyingine ambayo itakayompatia kipato tofauti na uhalifu.

Akizungumzia kuimba na wabongo msanii huyo alisema kwamba alikutana a Ay, Mwana FA na Jaffarai katika Klabu Maisha na kwamba wamekubaliana kufanya nyimbo kabla hajarudi Marekani ambayo tayari ameanza kuifanyia kazi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents