GOOD NEWS: DStv wairejesha Ligi kuu soka Italia ‘Serie A’ kwenye ving’amuzi vyao (+video)

Kampuni ya MultiChoice Tanzania imetangaza habari njema kwa watumiaji  wake wa ving’amuzi vya DStv ambapo wairejesha tena Ligi Kuu Soka ya Italia ‘Serie A’ .

Kuanzia msimu huu mpya wa 2018/19 DStv wataanza kurusha mechi zote za ligi hiyo kongwe duniani na wameahidi kuonesha zaidi ya mechi 1200 katika msimu huu mpya wa soka.

Hamasa ya DStv kufanya hivyo imekuja baada ya mchezaji bora duniani kwa mara tatu mfululizo Cristiano Ronaldo kutimkia kunako klabu ya Juventus.

Msimu mpya wa soka umewadia na Multichoice Tanzania imetangaza kurusha zaidi ya mechi 1200 kupitia vifurushi vyetu,kunogesha mambo zaidi,Ligi kuu ya Italia marufu kama Serie A imerejeshwa na kama Mteja wa DStv utapata fursa ya kutazama mechi zote za Ligi hiyo. Mbali na habari za kurudi kwa Serie A, pia tumeongeza maudhui zaidi katika soka msimu huu. Watumiaji wa DStv Bomba, wataweza kuona zaidi ya mechi 108 katika michuano ya  Serie A na Ligi Kuu ya Uingereza, huku wateja wa DStv Family wao watakuwa wakipata mechi zote 380 za michuano ya Serie A na mechi zaidi ya 120 kutoka Ligi Kuu ya Uingereza. Watumiaji wa kifurushi cha DStv Compact, Compact Plus na wateja wa Premium watakuwa na upatikanaji wa mechi zote za Kiingereza Premium League, Serie A na mechi zote 380 za La Liga.“amesema Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Mria.

 

 

 

Related Articles

4 Comments

Bongo5

FREE
VIEW