DStv Inogilee!

Goodluck Gozbert (Lollipop) aachia album yake mpya ‘IPo Siku’

Muimbaji, mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji wa muziki, Goodluck Gozbert ambaye pia anafahamika kwa jina la Lollipop ameachia rasmi album yake mpya iitwayo ‘Ipo Siku’.

Lolly

Goodluck ambaye mwishoni mwa mwaka 2015 alishinda tuzo ya ‘Wimbo Wa Mwaka’ kwenye Xtreem Awards za nchini Kenya, amesema album yake yenye nyimbo nane imeingia sokoni Alhamisi ya January 14, 2016 na inasambazwa na kampuni ya Msama Promoshens.

Lolli album

Miongoni mwa nyimbo zinazopatikana kwenye album hiyo ni pamoja na ‘Ipo Siku’ na ‘Acha Waambiane’ ambazo ziliachiwa kwenye vituo vya redio toka mwaka jana. Nyingine ni ‘Hao Hao’, ‘Nimesamehe’, ‘Pendo Langu’, ‘Moyo Tulia’ na ‘Surprise’.

Lollipop ndiye mwandishi wa nyimbo za wasanii wa Bongo fleva kama ‘Siachani Nawe’ na ‘Nivumilie’ za Barakah Da Prince, pamoja na ‘Basi Nenda’ na ‘Nitazoea’ za Mo Music.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW