Habari

Google yawatimua kazi watu 48 wakiwemo maafisa wake wakuu kwa tuhuma hizi

Kampuni ya teknolojia ya Google imewafuta kazi watu 48 wakiwemo maafisa 13 wakuu kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kingono tangu 2016.

Kwa mujibu wa BBC, Katika barua kwa wafanyakazi wake, mkurugenzi mmkuu mtendaji Sundar Pichai amesema kampuni hiyo kubwa ya teknolojia inachukua ‘msimamo mkali’ dhidi ya tabia zisizo sawa.

Barua hiyo inafuata ripoti ya New York Times kwamba muasisi wa mfumo wa Android Andy Rubin alipokea $90m kama kititia cha kuondoka licha ya kukabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu.

Msemaji wa Bwana Rubin alikana tuhuma hizo, gazeti hilo limesema.

Sam Singer amesema Bwana Rubin aliamua kuondoka Google mnamo 2014 kuanzisha kampuni yake ya teknolojia kwa jina Playground.

‘Aliagwa kama shujaa’ wakati alipoondoka, gazeti hilo linasema.

Barua ya Pichai inasema ripoti ya New York Times ni “ngumu kuisoma” na kwamba Google “inachukulia kwa uzito” suala la kutoa “nafasi salama ya kazi na inayotoa fursa kwa usawa”.

Andy RubinMuasisi wa mfumo wa Android Andy Rubin aliondoka Google mnamo 2014

“Tunataka tuwahakikishie kwamba tunatathmini malalamiko yote kuhusu unyanyasaji wa kingono au utovu wowote wa nidhamu, tunachunguza na tunachukua hatua,” aliendelea.

Hakuna mfanyakazi aliyetimuliwa katika miaka miwili iliyopita aliyepokea kitita cha kuondoka Pichai ameongeza.

Kwa mujibu wa ripoti ya New York Times, wakurugenzi wawili wa Google, wameeleza kuwa aliyekuwa mkurugenzi mkuu mtendaji Larry Page aliomuamba bwana Rubin kujiuzulu baada ya kampuni hiyo kuthibitisha malalamiko ya mfanyakazi mwanamke kuhusu tnedo la ndoa lililofanyika katika chumba cha hoteli moja mnamo 2013.

Rubin alisema hakufanya utovu wowote wa nidhamu na aliondoka Google kwa hiari yake.Google headquarters in Hamburg

Tuhuma hizi zinaongezea malalamiko kuhusu kukanwa kwa utamaduni ulioko unaoshinikiza unyanyasaji wa kingono katika kampuni hiyo iliyo na idadi kubwa ya wanaume.

Hisa za Alphabet, inayoimiliki kampuni ya Google, zimeshuka kwa zaidi ya 3% New York baada ya kutangaza mapato ya $33.7bn kwa miezi mitatu hadi Septemba – kiwango kilicho chini kidogo na kilichotarajiwa na wacahambuzi.

Hatahivyo faida jumla ilikwea kutoka $2.5bn hadi $9.2bn – kiwango cha juu zaidi ya ilivyotarajiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents