Michezo

Gor Mahia yaifuata Everton England, yaagwa uwanja wa Ndege wa Kenya (JKIA)

Kikosi cha klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya kimesafiri asubuhi ya leo kuelekea England kwaajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Everton.

Wachezaji wa Gor Mahia walikuwa kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata jijini Nairobi wakiwa tayari kwa safari ya kuelekea England.

Gor Mahia ambao ni mabingwa wa SportPesa Super Cup wamepata nafasi hiyo ya kuwakabili Everton baada ya kuwafunga mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC jumla ya mabao 2 – 1 kwenye mchezo wa fainali ya michuano hiyo iliyopigwa Juni 10, 2018.

Kwa mujibu wa mtandao wao wa kijamii Gor Mahia itawavaa Everton Novemba 6, 2018 mchezo utakao kuwa mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya Kenya pamoja na mitandao ya YouTube na Facebook.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents