Michezo

Greg Rutherford ajiondoa michuano ya London

Mwanamichezo raia wa Uingereza, Greg Rutherford amejiondoa katika michuano ya dunia ya kuruka viunzi inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mjini London kutokana na kupata maumivu ya kifundo cha mguu.

Rutherford aliyeshinda medali ya dhahabu kwenye mbio za Olyimpiki mjini London mwaka 2012, amesema anasikitika sana kukosa nafasi hiyo muhimu.

LakiniShara Proctor, Jazmin Sawyers, Lennie Waite, Marc Scott na Jess Turner kwa pamoja wamejumuishwa kwenye kikosi hicho huku, Richard Kilty, ambaye alitarajiwa kuchukua nafasi ya Rutherford nae pia amejiondoa kwa sababu ya maumivu ya kidole cha mguu.

Michuano hiyo ya dunia inatarajiwa kuanza Agosti 4 mapa 13 mjini London.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents