DStv Inogilee!

Guardiola aitaka Bayern kuifunga Liverpool Champions League ‘Waingereza mtanisamehe, naipenda Bayern’

Meneja wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola anamatumaini makubwa waajiri wake wa zamani Bayern Munich wataweza kuwafunga Liverpool na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Champions League.

Guardiola ameyasema hayo mara baada ya kutoka kuwashushia kipigo kikali klabu ya Schalke cha jumla ya mabao 7 – 0 na hivyo kufanya kuwa na ‘aggregate’ ya jumla ya magoli 10 – 2 na kufanikiwa kusonga mbele hatua ya robo fainali ambapo imeungana na Spurs pamoja na Man United kutoka Uingereza ambazo zilishajikatia tiketi mapema juma lililopita.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Sky Sports , kitendo cha Man City kutinga hatua hiyo ya robo fainali ya Champions League kunafanya jumla ya timu tatu za Uingereza kuwa kwenye hatua hiyo jambo ambalo kwa mara ya mwisho kwa klabu za nchi hiyo kufanikiwa kufanya hivyo ilikuwa ni mwaka 2010/11.

Kama Liverpool itashinda mchezo huo dhidi ya Munich itafanya timu kutoka Uingereza kufikia nne zilizofanikiwa kutinga hatua ya robo fainali.

“Samahani kwa watu wa Uingereza lakini naihtaji Bayern isonge mbele,” amesema Guardiola.

Pep Guardiola ameongeza “Mimi ni sehemu ya klabu hii. Naipenda Munich. Naipenda Bayern, ninamarafiki wengi kule.”

Akiuzungumzia mechi wake dhid ya Schalke, Guardiola amesema katika dakika 20-25 za awali walikuwa wanacheza ili kulinda matokeo waliyopata kwenye mchezo uliyopita huko nchini Ujerumani na hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya wao kutoshambulia.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW