Michezo

Guardiola amtolea uvivu, Mourinho ”Kuna makocha wengi bora na hawajashinda makombe’ 

Meneja wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa kamwe hatamhukumu, Jose Mourinho kwa kauli yake aliyo waambia waandishi wa habari kumpatia heshima yake kwa kuwa ametwaa mataji matatu ya ligi kuu England kuliko kocha mwingine yoyote waliyopo sasa.

Kauli hiyo ya Mourinho imejiri baada ya kupoteza mfululizo kwenye michezo yake ya mwanzo wa ligi mbele ya Brighton na Tottenham. Wakati meneja wa Manchester City, Guardiola alipoulizwa juu ya kauli hiyo ya Mourinho amesema kuwa hawezi kuukumu hilo.

Kocha Pep Guardiola akiwa amekumbatiana na Jose Mourinho baada ya mchezo wao

”Siwezi kuukumu hilo isipokuwa wapo makocha wengi waliyo bora na hawaja fanikiwa kushinda mataji ndiyo maana kwa upande wanguna naweza kusema inatokea kushinda kwakuwa unakitu cha ziada kinachokufanya ufanikiwe hilo, hata hao mameneja wazuri wanashindwa kushinda ubingwa kutokana na hicho kitu cha ziada kukosa kama vile klabu nzuri yenye wachezaji waliyo na viwango vya hali ya juu,” amesema Guardiola.

Pep Guardiola ameongeza “Nimelisema hilo mara kadhaa kwa mfano hata mimi mwenyewe nimeshinda mataji kwa sababu nilikuwa kwenye klabu kubwa zenye wachezaji bora na kama hilo lisingekuwa nisingeshinda hata ubingwa.” Hata hivyo Mhispania huyo hakusita kumpa heshima yake Mourinho kwakusema kuwa hakuwahi kuwa na shaka na ubora wake hivyo hata leo itaendelea kuwa hivyo lakini siyo kwa sababu ya mataji tu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents