Michezo

Guardiola, Kane na Hazard washinda tuzo za EPL

Kocha wa klabu ya soka ya Manchester City, Pep Guardiola ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi Februari katika ligi ya Uingereza.

Guardiola ameshinda tuzo hiyo baada ya timu yake kufanya vizuri katika michezo ya ligi waliocheza ndani ya mwezi huo na kupata matokeo mazuri ikiwemo 4-0 West Ham (ugenini), 2-1 dhidi ya Swansea (nyumbani) na 2-0 dhidi ya Bournemouth (ugenini).

Naye Harry Kane wa Tottenham Hospurs amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kwenye ligi hiyo.

Wakati huo huo Eden Hazard wa Chelsea kupitia goli lake la pili alilofunga kwenye mchezo wao dhidi ya Arsenal limefanikiwa kushinda tuzo ya goli bora la mwezi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents