Michezo

Guliyev ambwaga bingwa wadunia mita 200 London

By  | 

Mwanariadha raia wa Uturuki, Ramil Guliyev ameshinda mbio za dunia za mita 200, baada ya kumshinda bingwa wa dunia wa mita 400, Wayde van Niekerk raia Afrika Kusini aliyeshika nafasi ya pili na Isaac Makwala kutoka Botswana akishika nafasi ya tatu katika michuano hiyo mikubwa duniani inayoendelea Jijini London.

Mwanariadha raia wa Uturuki, Ramil Guliyev

Van Niekerk alihitaji kuweka histori katika mashindano hayo kwa kunyakuwa ubingwa wa mbio za 200m na 400m kwa wakati mmoja kama alivyo wahi kufanya mkimbiza upepo, Michael Johnson miaka 22 iliyopita lakini ameshindwa na kuambulia nafasi ya Pili katika mbio hizo.

Guliyev mwenye umri wa miaka 27, amesema kuwa alikabiliana na upinzani mkali wa Van Niekerk (aliyetumia sekunde 20.11) na Jereem Richards wa Trinidad na Tobago waliyo tumia (20.11), na kuishindia nchi yake Medali ya dhahabu kwa mara yake ya kwanza akiwa ametumia muda wa 20.09 katika mashindano yanayoendelea Jijini London

Guliyev  amesema kuwa ” Matokeo haya hayajanishitua lakini kama siamini”,  amesema Ramil Guliyev.

Ramil Guliyev ameongeza kwakusema kuwa “Nimeonyesha uwezo wangu katika mashindano haya. Nina stahili nilichokipata na nina furaha sana kuwa bingwa wa dunia na hiki nikipindi changu kizuri ambacho sitakuja kukisahahu”.

By Hamza Fumo

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments