Bongo Movie

Gumzo la jiji: Mwigizaji Kajala afungwa Segerea!!


Aliyewahi kuwa Mrs. Majani, malkia wa Bongo Records na sasa Bongo Movie actress Kajala Masanja, mapema leo amechukuliwa na kufungwa Segerea kufuatia mashitaka ya ufujaji wa pesa za umma zinazomkabili yeye pamoja na mume wake wa sasa hivi.

Kesi hiyo ambayo imekuwa ikisikilizwa kwa muda mrefu sasa inaonekana kufikia hatua za mwisho baada ya hakimu kusemekana kutoa hukumu Jumatatu ya tarehe 19 Machi mwaka huu.

Kajala ambaye ana watoto na P-Funk, hivi sasa yuko Segerea akisubiri hukumu yake kusomwa baada ya siku hizi chache. Washikaji zake wametoa tamko mbalimbali kupitia blogs, BBM na Facebook za kumuombea uzima na uwezo wa kuepuka kifungo.

Bongo5 inaendelea na taratibu za kupata usemaji wa P-Funk na wadau wengine kuhusu hii ishu ambapo tutazidi kukuletea yatakayojiri.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents