Burudani

H.Baba na Flora Mvungi wanatarajia mtoto, watampa aka ‘Tanzanite’

Familia za wasanii wa Tanzania zinaendelea kukua. Baada ya Mabeste na Lisa kupata mtoto wa kiume jana waliyempa jina Kendrick, Hamis aka H.Baba na muigizaji wa filamu Flora Mvungi nao wanatarajia kupata mtoto wao hivi karibuni.

12

Leo H.Baba ameonekana kwenye hospitali ya Marie Stopes jijini Dar es Salaam, akiwa amemsindikiza mke wake kwenda kuangalia kichanga chao kinaendeleaje tumboni.

“Tupo tunamchungulia dogo kuangalia anaendeleaje,” H.Baba ameiambia Bongo5.

“Bado hivi kidogo, tumeangalia anaendelea naona yuko fresh.”

Hamis amesema tayari wameshampa mtoto wao jina la kisanii ambalo ni Tanzanite.

“Huyu ndio Tanzanite sasa original. Unajua rasilimali za Tanzania inabidi tuzitangaze sababu mtu anapokuja akisikia dogo anaitwa Tanzanite inakuwa rahisi sana kuliko mambo ya kutaja vitu vingine,” amesema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents