Habari

Hacker wa Marekani watuhumiwa kuuteka mtandao wa takwimu wa Australia

Wahalifu wa mitandao ya kijamii maarufu kama hackers wamedaiwa kuufunga mtandao wa ofisi ya takwimu ya nchini Australia.

how-to-become-a-hacker-735x400

Waziri mkuu wa nchi hiyo Malcolm Turnbull amesema kuwa mtandao huo wa takwimu wa nchi hiyo umefungwa na wahalifu hao wanaodaiwa kutokea nchini Marekani.

“Siyo rahisi kupata takwimu sahihi hasa kama unatumia mifumo tofauti na inayotumika katika sehemu nyingine jambo hili limetokea kwa wakati ambao halikutarajiwa na linafanya watu kukosa takwimu,” alisema Waziri huyo.

Waziri huyo pia ameongeza kuwa japo taarifa za mitandao kuonyesha kuwa hackers hao wapo nchini Marekani lakini pia hawawezi kusema moja kwa moja watu hao wapo Marekani na hivyo bado wanafanya juhudi kuona kama wanaweza kurudisha mtandao huo.

Marekani ni nchi ambayo inatuhumiwa na nchi nyingi duniani kwa kuteka na kunakiri siri za mitandao ya mataifa mengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents