Bongo Movie

Haina haja ya kuleana kwenye maisha – Irene uwoya

Msanii wa Filamu Bongo, Irene Uwoya amefunguka kuhusu tabia ya baadhi ya wanawake kutopenda mafanikio ya wazao badala yake wapo tayari kushuhudia wenzao wakishindwa.

Muigizaji huyo amesema watu wa aina hiyo hakuna haja ya kuwa nao katika maisha ya kila siku na yeye kila siku anawapunguza katika maisha yake kwani amegundua wanawake wengi hawapendani.

“Hivi kwanini wanawake tunakuwa hatupendani??? yaani najiulizaga sanaaa, badala sisi tushirikiane ndio kwanza tunarudishana nyuma, mtu akifanya kitu kizuri au biashara ndo kwanza kuponda,” ameandika Irene Instagram na kuendelea.

“Ukifanya mabaya ndo anakusifia ili uwendeleee kuharibu, halafu yeye akifanya lake anataka umuunge mkono anasahau yeye hakuwahi kufanya hivyo, sasa hivi nimeamua si support mtu yeyote asiye ni-support, na haina haja ya kuleana kabisa mtu asiye kuwa na umuhimu kwenye maisha yako haina haja ya kuwa sehemu ya maisha yako atakurudisha nyuma tuu,” amesisitiza.

Irene amemaliza kwa kushauri wanawake waachane na marafiki wanaowashauri kuhusu starehe pekee siku zote badala yake wakae na marafiki ambao watawashauri namna ya kuingiza fedha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents