Habari

Haitham bin Tariq Al Said ambaye ni binamu wa Qaboos, ameteuliwa kuwa Sultan mpya wa Oman baada ya kifo cha aliyekuwa Sultan Qaboos bin Said – Video

Haitham bin Tariq Al Said ambaye ni binamu wa Qaboos, ameteuliwa kuwa Sultan mpya wa Oman baada ya kifo cha aliyekuwa Sultan Qaboos bin Said

Haitham bin Tariq Al Said ambaye ni binamu wa Qaboos, ameteuliwa kuwa Sultan mpya wa Oman baada ya kifo cha aliyekuwa Sultan Qaboos bin Said. Haitham alikuwa Waziri wa Utamaduni, wakati wa uongozi wa Qaboos. Sultan wa Oman Qaboos bin Said amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Taarifa ya kifo cha Qaboos imetolewa na TV ya taifa ambapo pia zimetangazwa siku 3 za maombolezo pamoja na siku 40 za bendera kupepea nusu mlingoti. Sultan Qaboos amefariki akiwa na umri wa miaka 79.

Sultan wa Oman, Qaboos bin Said amefariki dunia Januari 10, 2020 akiwa na miaka 79. Qaboos alikuwa mmoja wa viongozi walioongoza kwa muda mrefu zaidi Mashariki ya Kati ambapo alitwaa uongozi mwaka 1970. Chanzo cha kifo chake hakijabainishwa, lakini alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu.

https://www.instagram.com/p/B7K_swxhB1v/

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents