Michezo

Haji Manara aanika ukweli wake juu ya Tshishimbi ”Huwezi kujua ya kesho” (+AUDIO)

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameweka ukweli wake hadharani kuwa anakosha na kazi ya kiungo mkabaji wa Young Africans Sports Club, Papy Tshishimbi na kusema kuwa hata yeye anapenda kumuona mchezaji huyo Msimbazi.

Haji Manara na Papy Tshishimbi

Hivi karibuni zimesambaa taarifa mbalimbali katika mitandao ya kijamii kwamba kiungo huyo yupo njiani kuondoka katika klabu ya Yanga, huku mkataba wake ukiwa ukingoni kumalizika msimu huu.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram, Haji Manara amesema kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa mchezaji huyo na anapenda kumuona siku moja akiichezea Simba.

Box to box midfielder’ Papy Tshishimbi, siyo siri mimi ninamshabikia sana. Nikiulizwa natamani siku moja aje kucheza Simba, Yes napenda iwe hivyo ila kwa sasa bado ni mchezaji wa Gongowazi, lakini huwezi kujua ya kesho“, amesema Manara.

Mchezaji mwenyewe Tshishimbi amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na klabu yoyote ambayo itafikia makubaliano naye. Mpaka sasa imebakia miezi takribani minne mkataba wa mchezaji huyo kumalizika katika klabu ya Yanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents