Haji Manara afunguka kutua kwa kocha mpya wa Simba Mbelgiji

Kumekuwa na maneno ya hapa na pale kuhusu kutua nchini kwa kocha mpya wa mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba raia wa Ubelgiji, Patrick Aussems afisa habari wa timu hiyo, Haji Manara amegusia jambo hilo pale alipofanya mahojiano na radio EFM.

Wakati wapenzi, mashabiki na wadau wa soka nchini wakisubiria kwa hamu kufahamu ukweli juu ya kutua kwa kocha huyo Mbelgiji, Patrick Aussems aliyeonekama uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere akiwa na Katibu Mkuu wa Simba Dkt Arnold Kashembe siku ya Jumapili, Manara amesema kuwa muda bado haujafika wa kulizungumzia hilo.

“Itakapo kuwa imethibitika kuwa ni kocha wa Simba basi tutalisema, pale itakapo bidi kusema tutasema. Kwa sasa hivi tutambue Simba inaongozwa na kocha msaidizi ‘Assistant Coach’ Irambona Masud Juma,” amesema Manara wakati akifanyiwa mahojiano na radio ya EFM.

Haji ameongeza “Mawazo yetu kwa sasa yapo kwenye michuano ya kombe la KAGAME Cup, hivyo muda utakapo fika tutalizungumza hilo.”

Mbelgiji, Aussems mwenye umri wa miaka 53 anatarajiwa kurithi mikoba ya Mfaransa wa Simba SC, Pierre Lechantre huku akiwa na hiztoria ya kuzinoa timu zinazoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa kama ES Toyes AC na Stade de Reims, AC Leopards walati timu ya mwisho kuifundisha ikiwa ni Napel mwaka msimu wa mwaka 2015/16.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW